Wednesday, March 25, 2009

BILLY GRAHAM AND US PRESIDENTS!

David Frost ndiye muandishi, ni habari inayoeleza nyuma miaka 30 Mazungumzo yao na Billy Graham katika kitabu kiitwacho “Personal thoughts of a public man”

Billy Graham ni mhubiri wa kimataifa, anafahamu siasa za Marekani na amekuwa rafiki wa karibu wa karibu kila raisi wa taifa hilo kubwa kama vile,Harry Truman, Eisenhower, Lyndon Johnson ,John Kennedy, Richard Nixon na Bill Clinton.

Ukurasa wa 95
President Bill Clinton, May 6, 1996 alinukuliwa akisema:

‘I hardly ever go to a place, as Presiident, that Billy Graham has not been there before me preaching. And I feel like a poor substitute, because a lot of the time what I’m trying to do is to get people to lay down the hatred of the heart and reach down into their spirit and treat people who are different from themselves with the same respect that all God’s children are entitled to…………………..
I thank Billy and Ruth Graham for the ministry of their lives’

Ukurasa wa 97;

David Frost, mwandishi wa kitabu hichio: anasema ‘No preacher in the history of this country has had so much access to many presidents as Billy Graham’.



Hapana shaka kuwa alikuwa mshauri wa kisiasa wa wakuu hawa wa Marekani, ushauri uliobeba ukweli na sera zenye kubeba haki na demokrasia.

Marekani ya leo inayoongozwa na Rais Obama, mweusi, ni dhahiri kuwa ni mwendelezo wa harakati fulani za hadharani kama za kina Martin Luther na kina Billy Graham.`

Hapa tunajifunza kuwa viongozi waongozao roho zetu wana nafasi kubwa ku ‘influence’ siasa zetu, hapa Afrika na hasa Tanzania katika kujenga jamii bora zaidi,yenye hofu ya Mungu na kusimamia haki. Na si kuendekeza ufisadi unaolimaliza bara la Afrika. Mfano mzuri wa mapambano haya na harakati za kuipigania haki ni Askofu Desmon Tutu wa Afrika ya kusini. Ambaye wakati Mandela akiwa gerezania alionekana hadharani akiongoza maandamano ya kuidai haki ya usawa ndani ya nchi yao na kuna wakati aliwakemea watawala wa Afrika a kusini, wabaguzi,, kwa sauti kuuuubwa “ Release our leaders”, “Release our leaders”, “Release our leaders”. Bado watanzania tumo katika kifungo cha umasikini, maradhi, ujinga, ufisadi. Nani wapigao kelele mithili ya Desmond Tutu akiwataka watawala wetu na wakoloni wetu wa kale kutuacha huru.


Wako wapi kina Billy Graham wetu Tanzania!

2 comments:

Anonymous said...

Nakubaliana na maneno yako kaka. Billy Graham ana ujiko usio wa kawaida hapa Marekani. Maktaba yake hapa Charlotte,NC sio ya kawaida.

Anonymous said...

Billy Graham ananivutia sana!, kuna wakati aliweka wazi kuwa yeye ni Democrat!,Hapa kwetu viongozi wa dini bado hawajaweza kuwa wazi misimamo yao kisiasa, hata tu kusema chama fulani kina sera nzuri kinaweza kulisaidia taifa letu.Nadhani bado kuna kaunafiki fulani.