Saturday, April 4, 2009

SIJUI NIJARIBU UBUNGE?


Wapo wanaosema ndogo, wapo wanaosema zinatosha, wapo wanaosema ziko juu sana. Hata wao wenyewe wanatofautiana mfano ni 'ishu' hiyo hapo juu kama ilivyoelezwa na mbunge wa Karatu Dr. Slaa.
Mi nasema ni nyingi mno ukizingatia mishahara ya watu wetu bado iko chini sana, fikiria pale wahutimu wa vyuo vikuu wanaolipwa mshahara wa laki tatu na nusu. Kwa mbunge anayepata 6,900,000/= kwa mwezi kipato chake ni sawa karibu mara ishirini ya kipato anachopata mhitimu wa chuo kikuu.
Kwa maelezo yoyote yale,hii si sawa!

2 comments:

ndesanjo said...

Pius,
Naona wananchi wote basi tuwe wabunge! Au unasemaje?

Pius said...

Ndiko kwenye ulaji kaka, tena tumechelewa, si unaona kina Dr. nanihii, Prof. nanihii, mwalimu nanihii, Engineer nanihii na kina nanihii wengine wenye taaluma nanihii wote wamekimbilia huko.