Karibuni wote
Nawakaribisha katika blogu hii tuweze kendeleza harakati za kujikomboa dhidi ya maadui watuzungukao yaani ujinga, maradhi na umaskini pamoja na kila aina ya ufisadi unaoendelezwa na mafisadi ndani ya mfumo wa kifisadi.
Mapambano hayajaisha kwani ukoloni unaendelezwa kupitia mlango wa nyuma na unyonyaji bado ungalipo.Mtu duni anaendelea kuwa duni na mwenye nacho anaendelea kuwa nacho kwa kumnyonya mtu duni asiye na sauti.Bila usawa hakuna haki. Ni jukumu letu sote kuupigania usawa ndani ya jamii tuishiyo kwani binadamu wote ni sawa na wote tuna haki ya kuishi maisha bora.
Sunday, June 24, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Tumeshakaribia Mzee Pius.
Nakushukuru Da'mija kwa kunitembelea.
Pia ninakupongeza sana kwa ushindi wa kimbunga ulioupata.Ninaamini tuna viongozi wenye nguvu na hamna sababu ya kuwa na jumuiya dhaifu.
Nia ipo, uwezo upo, sababu zipo, kwa nini tusisonge mbele?
Kila la kheri.
Post a Comment