Thursday, June 28, 2007

FRIJI ISIYOTUMIA UMEME

Hii ni habari njema.Habari hii nimeipata kutoka idhaa ya kiswahili BBC.Ni teknolojia itakayotuwezesha kutumia vyombo vya kupoozea kama vile friji bila ya kutumia umeme.Kilichonivutia zaidi, teknolojia hii ilikuwa ikiongelewa na mtanzania mwenzetu aliyefanya utafiti wake nchini Uingereza.Mwandishi wa habari wa BBC alipomuuliza mhandisi huyu,tarehe 13th March 2007, kuwa kwa nini akiwa kama mwafrika asiisaidie nchi yake kuileta teknolojia hii.

Anamjibu,

“Endapo viongozi wetu na watunga sera watataka kupata utaalamu wangu ili uinufaishe nchi yetu niko tayari”

Swali ninalojiuliza ni kwamba, ni kwa nini hawa tuliowapa dhmana ya kutuongoza hawana mikakati madhubuti na endelevu ya kuwatumia wataalamu wetu walioko ughaibuni hata waliopo nyumbani kwa manufa ya nchi yetu?

Je ni ubutu wa fikra?

Je ni kutokujua?

Au ni nini hasa?

Kuongoza ni kuonyesha njia. Kila mmoja atimize wajibu wake

2 comments:

luihamu said...

Mzee Pius karibu,unakaribishwa sana.Natumai tutakuwa wote pamoja.




Jah bless.

Pius Ntwale said...

Luihamu nakushukuru sana kwa kunitembelea.
Naam tupo pamoja mzee!

Luihamu na wanablogu wote, hapa nilipo jamaa wanapiga stori, nchi hii kila mtu ni ku-figth mwenyewe,mradi unapata mlo wa siku, viongozi wetu kila mmoja ni msanii tu!,kweli jamii yetu imekata tamaa!.Inahitaji muelekeo mpya.Nadhani kuna haja kuwa na jumuiya yenye nguvu kabisa ili tuisaidie nchi yetu.Kuna haja ya kuwa na mjadala utakaolenga kutung'oa hapa tulipo.
Mungu ibariki Tanzania!
Mungu tuepushe na mafisadi wanaoiharibu nchi yetu!